26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Stamina azidi kuianika ndoa yake

Beatrice Kaiza

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini, Boniveture Kabogo, Stamina ameamua kuandika Makala inayoelezea kisa na mkasa wa ndoa yake.

Msanii huyo baada ya kuachana na mke wake akaamua kuachia wimbo unaojulikana kwa jina la Asiwaze ukiwa unaanika kile kilichotokea kwenye ndoa yake.

Stamina amedai mbali na kuachia wimbo huo, lakini ameona bora aandike Makala na kuweka wazi kile anachokijua yeye kwenye maisha ya ndoa.

“Wewe unaweza kua una uelewa mkubwa kuliko hata mimi kwenye maswala ya ndoa ila mimi nimeona niandike kivuli cha ndoa hasa kwa kile ninacho kifahamu ili kubadilishana mawazo, kufundishana na kuburudishana kama ilivyo lengo la fasihi simulizi na fasihi andishi ukisoma nina imani utachanganya na mawazo yako,” alisema Stamina.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,628FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles