25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rihanna aogopa kupanda helikopta

Los Angeles, Marekani

MSANII wa muziki na mitindo nchini Marekani, Rihanna Fenty, ameweka wazi kuwa, tangu kifo cha nyota wa mpira wa kikapu nchini humo Kobe Bryant, anaogopa kupanda helikopta.

Bryant alipoteza maisha Januari 26 kwa ajili ya helikopta huku akiwa na mtoto wake wa kike Gianna pamoja na watu wengine saba.

Kutokana na tukio hilo lililotikisa dunia, Rihanna amedai hadi sasa amekuwa akiogopa usafiri huo japokuwa awali alikuwa anautumia mara kwa mara.

“Mimi ni msanii pia ni mfanya biashara, muda mwingi nilikuwa natumia usafiri wa helikopta, lakini tangu Kobe Bryant apate ajari na kupoteza maisha nimekuwa nikiogopa kuutumia usafi huo, namkumbuka sana staa huyo wa kikapu, nitaendelea kuwaombea watoto waliobaki pamoja na mama yao Vanessa,” alisema msanii huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles