24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Sri Lanka yafukuza wahubiri 200 wa Kiislamu

COLOMBO, SRI LANKA

MAMLAKA za Sri Lanka zimewafukuza wageni zaidi ya 600 wakiwemo wahubiri karibu 200 wa Kiislamu, tangu kutokea kwa mashambulizi ya Pasaka ya kujitoa mhanga.


Waziri wa Mambo ya Ndani, Vajira Abeywardena, amesema wahubiri hao waliingia nchini kihalali, lakini wakati wa msako baada ya mashambulizi hayo, waligundulika vibali vyao vimeisha muda.


Waziri huyo hakutaja majina wala nchi wanakotoka, lakini polisi wanasema wageni wengi ambao vibali vyao viliisha muda wanatoka Bangladesh, India, Maldives na Pakistan.


Kwa mujibu wa waziri huyo taifa hilo kwa sasa linapitia upya mfumo wa uombaji visa kufuatia hofu kuwa wahubiri hao wanaweza kueneza itikadi kali na kusababisha mashambulizi mengine.


Taifa hilo limetangaza hali ya hatari tangu kutokea mashambulizi na kutoa mamlaka makubwa kwa vikosi vya usalama kumshikilia mtu na kumweka kizuizini kwa muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles