27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali yaelekeza macho Marekani kusaka wafadhili

NAIROBI, KENYA

BAADA ya kudaiwa kuambulia patupu katika ziara ya karibuni nchini China ilikoenda kuomba mkopo, Serikali ya Kenya kwa sasa inaelekeza nguvu nchini Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje, Monica Juma ataongoza ujumbe wa serikali katika ziara hiyo nchini Marekani kuanzia Jumanne hadi Jumatano.

Masuala ya ustawi wa kiuchumi, uwekezaji na vita dhidi ya ufisadi yanatazamiwa kupewa kipaumbele maafisa wakuu wa Kenya watakapokutana na wenzao wa Washington.

Kenya pia inatazamia kutafuta ushirikiano mkubwa zaidi utakaoboresha biashara zinazoendelezwa chini ya Sheria ya AGOA inayotoa nafasi za ustawi wa kibiashara Afrika.

Wiki chache zilizopita, ziara iliyofanywa na Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Chama cha ODM, Raila Odinga nchini China, iliripotiwa kuambulia patupu baada ya kunyimwa mkopo wa kufadhili ujenzi wa reli kisasa (SGR) kutoka Naivasha hadi Kisumu.

Ingawa hali hiyo ilionyesha ishara mbaya ya ushirikiano wa kibiashara kati ya Kenya na China ambao umekuwepo tangu Rais Kenyatta alipoingia madarakani 2013, serikali ilikanusha kwamba suala la ufadhili wa SGR lilijadiliwa wakati wa ziara hiyo.

Mkutano huo utafanyika siku chache tu baada ya  Juma kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza ambaye alizuru Kenya wiki iliyopita.

Aidha ziara ya Juma nchini Marekani inatokea pia siku chache baada ya Rais Kenyatta kufanya mabadiliko katika wizara hiyo kwa kubadilisha mabalozi mbalimbali akiwemo yule wa Kenya nchini Marekani.

Ijumaa iliyopita, serikali ilitangaza Robinson Githae ambaye alikuwa Balozi wa Kenya nchini Marekani kuwa balozi mpya nchini Austria kuchukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Michezo, Hassan Wario ambaye amesimamishwa kazi.

Balozi mpya wa Kenya nchini Marekani sasa atakuwa Bw Lazarus Amayo, ambaye kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles