22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 41 wauawa kwenye ajali ya ndege Moscow

Watu arubaini na moja wameuawa baada ya ndege ya Urusi kutua kwa dharura na kuwaka moto katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow.

Watoto wawili na mhudumu mmoja ni miongoni mwa waliofariki kwa mujibu wa vyombo vya habari Urusi.

Shahidi mmoja amesema ilikuwa ni “miujiza” kwamba kuna aliyenusurika mkasa huo wa ndege, iliyokuwa imebeba abiria 73 na maafisa wataano wa ndege.

Kwa mujibu wa Ofisa wa kamati ya uchunguzi, Yelena Markovskaya, watu 37 wamenusurika  katika ajali hiyo ambao ni abiria 33 na maafisa wanne wa ndege hiyo.

Taarifa pia zinasema watu watano wamepelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Aeroflot, shirika la ndege la kitaifa Urusi limesema ndege hiyo ililazimika kurudi katika uwanja wa ndege kutokana na sababu za kiufundi, lakini halikufafanua zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles