25.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

Solskjaer awatuliza mashabiki United

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa wavumilivu kutokana na mwenendo wa timu yao.

Kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Newcastle, Manchester United ilikuwa inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi, hivyo mashabiki wakaja juu kukuta na uongozi wa timu hiyo umfukuze kazi kocha huyo.

“Nani anajua safari yangu ya maisha ya soka? Nimepitia changamoto nyingi nikiwa mchezaji hadi kuwa kocha, kuna wakati nilikuwa natapata mafanikio nawakati mwingine mambo yanakuwa tofauti.

“Nilipata shida nikiwa Moldena Cardiff, kuna wakati timu zilikuwa zinamaliza nafasi ya mwisho jambo ambalo lilikuwa linaniumiza, naweza kusema huu ni wakati mgumu ambao tunaupitia, lakini muda mfupi mambo yatakuwa kwenye mstari, hivyo mashabiki wanataki wakuwa wavumilivu, najua inaumiza ila hali hiii tabadilika,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles