NBC kuwezesha wafanyabishara Singinda kusajili biashara zao Brela

0
573

Derick Milton, Singida

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), imezindua klabu ya wafanyabiashara wakubwa, wadogo na wakati katika mkoa wa Singida, lengo likiwa kuwawezesha wasajili biashara zao, kukata Bima, pamoja na kulipa Kodi.

Katika uzinduzi wa klabu hiyo Benki hiyo iliwakutanisha wafanyabishara na taasisi za kiserikali ikiwemo TRA, Brela, Bima pamoja na SIDO ili waweze kutengeneza mahusiano mazuri na kuboreshewa biashara zao.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati kutoka NBC Evance Luhimbo amesema kuwa benki hiyo imeamua kuunda klabu hiyo katika kuhakikisha wafanyabishara wananufaika na kazi yao.

“Kama benki tumeunda klabu hii lengo kubwa likiwa wafanyabishara wa aina zote wasajili biashara zao Brela, waweze kulipa kodi (TRA) kukatia Bima biashara zao na wajasliamali kupata msaada kutoka SIDO, tunataka kutengeneza mahusiano mazuri kati ya taasisi hizi na wafanyabishara,” amesema Luhimbo.

“Lakini tunajua wapo baadhi ya wafanyabishara hawajasajili biashara zao au hawana leseni na hawana elimu ya jinsi gani ya kufanya, kuwakutanisha hivi kupitia klabu itakuwa njia nzuri na sahihi kwa wafanyabishara kupata elimu hiyo,” ameongeza Luhimbo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Kizito amewataka wafanyabiashara hao kutumia klabu hiyo katika kuboresha biashara zao na kuzisajili huku akiitaka NBC kuongeza vituo vya kutolea huduma katika mkoa huo kwani vilivyopo ni 16.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here