29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Solskjaer amrudisha Cavani

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, ameibua taarifa njema kwa mashabiki wa timu hiyo akisema straika wao, Edinson Cavani, atarudi mzigoni siku chache zijazo.

Cavani (34), amecheza dakika 37 pekee msimu huu na majeraha yalisababisha aikose mechi ya wiki iliyopita, ambapo waliifunga Newcastle United mabao 4-1.

“Edi anatarajiwa kuunga na sisis hivi karibuni. Alikuwa fiti kwa mazoezi wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa, anapambana kurudi,” amesema Solskjaer akihojiwa na gazeti la Manchester Evening News.

Hata hivyo, Cavani atakayevaa jezi namba 21 baada ya ile ya namba 7 kumkabidhi Cristiano Ronaldo, hajasafiri na timu iliyoifuata Young Boys katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa usiku wa leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles