27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Pogba haendi PSG wala Madrid

KIUNGO wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba, hafikirii kuondoka Manchester United, licha ya saini yake kuwaniwa na PSG na Real Madrid.

Nyota huyo aliyetua Old Trafford mwaka 2016 akitokea Juventus, ambapo usajili wake wa Pauni milioni 89 ulivunja rekodi, amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Old Trafford, akihusishwa zaidi na klabu za PSG na Real Madrid.

Hata hivyo, taarifa mpya zimeibuka zikidai kwamba ‘mido’ huyo raia wa Ufaransa anataka kuongeza mkataba Old Trafford, akivutiwa zaidi na kiwango kizuri alichoanza nacho msimu huu.

Katika mechi nne za msimu huu wa Ligi Kuu ya England, Pogba anayehusishwa pia na klabu yake ya zamani, Juve, amechangia mabao saba kupitia pasi za za mwisho ‘asisti’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles