23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Sofia Richie, Kourtney Kardashian mambo shwali

CALIFORNIA, MAREKAN

HATIMAYE wanamitindo Sofia Richie na Kourtney Kardashian, wamemaliza tofauti zao baada ya kuwa kwenye mgogoro wa kipindi kirefu.

Kwa kuthibitisha hilo Sofia ameamua kumuomba urafiki mrembo huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram mrembo pamoja na ndugu zake katika familia ya Kardashian.

Wawili hao walikuwa hawaongei kwa muda mrefu baada ya Sofia kuingia kwenye mapenzi na Scott Disick ambaye alikuwa ni mume wa Kourtney na walifanikiwa kupata watoto watatu Mason Dash Disick, Reign Aston Disick na Penelope Scotland Disick.

Sofia mbali na kumuomba urafiki mrembo huyo, aliamua kuwaomba na ndugu wengine kutoka familia ya Kardashian ambao ni Kylie Jenner, Kim Kardashian na mama yao Kris Jenner, lakini Kendall Jenner na Khloe Kardashian hakuwajumuisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles