20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Gozbert awajibu mashabiki

Penda Hamisi, (TUDARCO)

MSANII wa muziki wa injili nchini, Goodluck Gozbert, amewajibu wale walioshangazwa na wimbo wake mpya wa Nibadilishe.

Video ya wimbo huo ambao ameuachia hivi karibuni, unaonesha mabadiliko makubwa ya aina ya muziki wake kutoka injili na kufananishwa na bongo fleva.

Msanii huyo amedai kazi ya msanii ni ubunifu, hivyo kazi zake nyingi amekuwa akitumia ubunifu wa aina mbalimbali ili kuwafikia mashabiki zake.

“Watu wamekua wakihoji sana aina ya uimbaji na ubunifu ninaotumia katika kazi zangu nyingi, kwenye ‘Nibadilishe’ jamii imeupokea kwa sura tofauti lakini ninaamini hakuna kosa lolote.

“Kwa wale ambao nimewakwaza naomba wanisamehe ila ninaamini watazoea na nitaendelea kutoa aina ya nyimbo kama hiyo kwa wingi zaidi,” alisema Goodluck.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles