Tunda Man awataka wasanii kuwekeza

0
977

GLORY MLAY

MSANII wa muziki wa bongo fleva, Khalid Ramadhani, maarufu kwa jina la Tunda Man, amesema asilimia kubwa ya wasanii wanaotegemea muziki maisha yao ni mabovu, hivyo wanatakiwa kuwekeza.

Msanii huyo amesema, wapo wasanii ambao wanategemea muziki na maisha yao yapo vizuri, lakini wapo wachache wa aina hiyo.

“Hauwezi kutegemea muziki peke yake ukasema utakuwa na maisha maziri, msanii anayejitambua lazima atafute na biashara nyingine hata kama muziki unalipa lakini hauwezi kufikia yale malengo ambayo umeyapanga ni wachache sana wenye bahati hiyo.

“Hivyo msanii anatakiwa kujiongeza, wengi tunawaona walivyoishia katika maisha mabaya kutokana na wao kuwekeza kwenye muziki pekee bila kujua maisha ya baadae yatakuwaje,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here