23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Rita Ora afunguka kuhusu Jay Z

NEW YORK, MAREKANI

ALIYEKUWA staa wa muziki kutoka kundi la Roc Nation, Rita Ora, ameweka wazi alihofia maisha yake ya muziki baada ya kugombana na mmiliki wa lebo hiyo Jay Z.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 28, aliwahi kusainiwa kwenye lebo hiyo mwaka 2008 kabla ya 2016 kuvunja mkataba wake. Amedai aliamua kuvunja mkataba huo kutokana na kunyanyaswa na kushindwa kupata nafasi kama wasanii wengine.

Kutokana na kitendo hicho walifikishana mahakamani ambapo Jay Z aliitaka mahakama kumfungia msanii huyo kufanya muziki kwa kipindi cha miaka mitano.

“Ukweli ni kwamba nilikuwa kwenye kipindi kigumu katika maisha yangu, muziki ni sehemu ya maisha yangu, nimekuwa nikiishi kwa kutegemea muziki sasa suala la kufungiwa miaka mitano lilinipa wasiwasi kubwa ya kuendesha maisha, hakuna kitu kingine ambacho ninakijua kama sio muziki, lakini ninashukuru kila kitu kilikwenda sawa na Jay Z akakubali kuyamaliza,” alisema mrembo huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles