MSANII wa kizazi kipya, Snura Mushi, ameweka wazi kwamba kama kazi za sanaa anazofanya hazitomwendea vema atarudi katika kazi yake ya ususi.
Snura alisema kazi hiyo anaimudu na kama hasingekuwa msanii angeitumikia hadi leo kwa kuwa haikuwahi kumwangusha kiuchumi.
“Nilikuwa msusi mzuri kiasi kwamba sikukosa wateja lakini kutokana na majukumu kunizidi katika sanaa ya muziki na maigizo nimeamua kuikacha kwa sasa lakini ipo siku nitairudia,” alisema.
Snura kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Najidabua’ aliouachia hivi karibuni, lakini pia aliwika na wimbo wake wa ‘Majanga’ na ‘Ushaharibu