MSANII wa muziki nchini Kenya, Charles Kanyi ‘Jaguar’, ameiomba Serikali nchini humo ianzishe mashindano ya shule ili iondoe muda wa wanafunzi kutumia dawa za kulevya.
Jaguar alisema vijana wengi wanaokimbia shule wanakimbilia vijiweni kwa sababu hakuna michezo lakini kama michezo itaanzishwa katika shule itaondoa wanafunzi kukimbilia vijiweni.
“Serikali iangalie jinsi ya kuanzisha michezo shuleni ili kuwafanya vijana wajiingize kwenye michezo hiyo badala ya kurudi mitaani na kuanza kutumia dawa za kulevya,” alisema Jaguar.
Msanii huyo aliyazungumza hayo juzi katika maafali ya nane ya chuo cha Mt Kenya University, huku akiwa mwakilishi wa chama cha kupinga matumizi ya dawa za kulevya Nacada.