Bobi Wine apata mtoto wa nne

0
1118

Bobi WineMSANII kutoka Uganda, Robert Kyagulanyi ‘Bobi Wine’ na mke wake, Barbie Kyagulanyi, wamepata mtoto wa kike anayetimiza jumla ya watoto wanne.

“Hii ni mipango ya Mungu, tunashukuru kwa dua zenu tumepata mtoto wa kike mwenye sura mzuri na hali ya mama yake inaendelea vizuri,” aliandika Bobi Wine kupitia akaunti yake ya Facebook.

Mashabiki wanasema kuwa huu ni mwaka wa watu maarufu na wasanii kupata watoto kama ilivyo kwa Nassib Abdul ‘Diamond’ kutoka nchini Tanzania, Jackie Matubia kutoka Kenya, Jua Cali kutoka Kenya, Mr Flavour kutoka Nigeria na wengine wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here