30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Smith: Ndoa yetu itakuwa ya mfano

will-smith-8-300NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa filamu na muziki nchini Marekani, Will Smith, amesema kuwa ndoa yake na mke wake, Jada Pinkett, itakuwa ya mfano kwa wasanii mbalimbali.

Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni, baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kwamba wawili hao hawana furaha katika ndoa yao na kuonyesha uwezekano mkubwa wa kuachana kwao.

Lakini Smith amesema, ndoa yake itakuwa ya mfano kwa wasanii na watu wengine kwa kuwa hadi sasa ina zaidi ya miaka 20.

“Nilifanikiwa kufunga ndoa miaka 20, lakini nashangaa kuona watu wakidai kwamba ndoa yetu ina mgogoro, lakini ukweli ni kwamba tuna furaha kubwa ya ndoa yetu na tutaendelea kuwa pamoja kwa miaka mingi.

“Hii itakuwa ni mfano wa kuigwa kwa wasanii na watu wengine ambao wanadhani kama tunaweza kuachana kwa sasa,” alisema Smith.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles