25.3 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Smile yazindua huduma mbili za mawasiliano

Pg 3NA FLORIAN MASINDE, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya mawasiliano ya Smile Tanzania imezindua huduma mpya mbili za mawasiliano zinazotumia mtandao wa intaneti wa 4G LTE.

Akizungumzia uzinduzi huo, Meneja Mkazi wa Kampuni ya Smile nchini, Eric Behner, alisema huduma hizo ni Smile Voice na Smile Unlimited.

Huduma ya Smile Voice itamwezesha mteja kupiga simu kwa njia ambayo ni ya kwanza nchini na yenye kusikika kwa ubora mkubwa.

“Huduma nyingine ni Smile Unlimited ambayo inatoa fursa kwa mteja kutumia huduma ya intaneti bila kikomo ndani ya siku 30,” alisema Behner.

Alisema kampuni ipo katika harakati za kuhakikisha wateja wake wanafikiwa kwa kupata huduma zenye ubora wa hali ya juu.

Aliongeza kuwa Smile Voice ni huduma ya hali ya juu inayopatikana kwenye vifaa vya Android na Apple iPhone tu kwa sasa, ya kumwezesha mteja kupiga simu mtandaoni kwa kutumia huduma ya vo LTE na kumpa uwezekano wa kusikika vizuri zaidi.

“Smile ni kampuni ya kwanza ya huduma za mawasiliano ya simu kuanzisha na kuendeleza programu ya bure ya huduma ya kupiga simu mtandao wa 4G LTE kutumia app,” alisema.

Aidha huduma hii inawawezesha wateja wenye simu za Android na iPhone kufurahia kupiga simu zenye ubora wa hali ya juu kupitia intaneti yetu yenye kasi zaidi.

“Tumejizatiti kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha tunaboresha huduma za kupiga simu kwa mtandao wa intaneti.

“Kwa kupitia huduma ya Smile Voice, wateja wetu wanaweza kupiga simu ndani na nje ya nchi kama mitandao mingine ya simu, lakini kwa kutumia data,” alisema Behner.

Aliongeza kuwa mbali na huduma ya Smile Voice, kampuni  imefanikiwa kutanua huduma zake za mtandao wa 4G LTE hadi kufikia miji saba nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles