29.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 6, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Mutungi akwepa ‘kikombe’ cha Zanzibar

mutungiNA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema hawezi kuzungumzia suala lolote linalohusu uchaguzi wa marudio wa Zanzibar unaotarajia kufanyika Machi 20.

Msajili alitoa msimamo huo jana baada ya kuulizwa swali na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu uhalali wa uchaguzi huo.

“Naomba mniepushe na kikombe hiki, naomba ndugu zangu mniepushe na hicho kikombe cha kuzungumzia masuala ya Zanzibar kwa undani, nadhani yatakuja kuzungumziwa zaidi kwenye Baraza la Siasa, lakini hivi sasa tujadili masuala yaliyotuleta ya maendeleo.

“Ninasema hivyo nikiwa na maana yangu kwa sababu ofisi yangu bado haijafika kujiridhisha kwenye hayo masuala yanayolalamikiwa na hata hili jina la Msajili linatunyima fursa ya kutetea vitu vingi, kukosa meno, na ikibidi wajumbe muangalie namna ya kulibadili ikibidi wapewe jina la Mratibu wa Siasa,” alisema Jaji Mutungi.

Jaji Mutungi aliitwa mbele ya kamati hiyo ili kuelezea uendelezaji wa miradi ya ofisi yake, huku wajumbe wa Zanzibar wakitumia nafasi hiyo kumtaka aelezee hatua alizozichukua kuhusu mabango ya uchochezi na vitisho vinavyoendelea visiwani Zanzibar.

Baadhi ya wajumbe hao kwa nyakati tofauti walisema mambo yanayofanyika hivi sasa visiwani humo hayana ishara nzuri na hayaleti picha kama itatokea uchaguzi ujao utafanyika kwa uhuru na haki, hivyo kumtaka aeleze hatua alizochukua hadi sasa.

Alisema anatamani kujibu hoja za wajumbe hao, lakini anaweza akawajibu kisiasa zaidi na yeye hapendi kugombana na wanasiasa kwakuwa kwa muda aliofanya nao kazi amewafahamu vya kutosha.

“Siku hizi nami nimekuwa mwanasiasa, ninaweza kuwapa hapa majibu ya kisiasa jambo ambalo si zuri,” alisema Jaji Mutungi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles