30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

‘SMARTPHONE’ ZINAATHIRI UHUSIANO KATI YA MZAZI NA MTOTO

NA AZIZA MASOUD,

UTANDAWAZI  ni moja ya vitu vinavyochangia kuathiri malezi ya watoto kwa kiasi kikubwa.

Wazazi wa miaka ya sasa wamekuwa na mambo mengi na hutumia muda mwingi katika vitu visivyo na msaada katika malezi ya watoto yakiwemo matumizi ya simu za kisasa ‘smartphone’.

Uwepo wa simu hizo ambazo zimeunganishwa na  mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo WhatsApp, facebook, instagram, imo, tango na twitter  unachangia wazazi  kukosa muda wa  kuwaangalia watoto wao.

Mbali ya kupata habari za matukio ya kila siku kupitia mitandao hiyo pia watumiaji hufanya mawasiliano na marafiki mbalimbali.

Mawasiliano mengi huwa ya mzaha, kutongozana na wakati mwingine kutupiana maneno makali.

Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao hiyo utakubaliana nami kwamba baadhi ya watu hukosa muda wa kuwaangalia watoto na hata kuangalia maendeleo yao ya shule.

Hakuna ubishi kuwa mitandao ya kijamii inaweza kumfanya mama au baba  kushindwa kuwa makini na familia.

Watoto wengi wa sasa wanapata madhara mbalimbali ikiwemo kuungua moto, kuanguka na kuvunjika baadhi ya viungo  kutokana na wazazi kutokuwa makini nao.

Wapo baadhi ya wazazi wamejiweka kando katika majukumu ya watoto wao na kuwaachia watumishi wa ndani huku muda mwingi wakiutumia kwa kuchati.

Siku za mapumziko si baba wala mama wote wako ‘busy’ kwa kuchati tu.

Kama mzazi unapaswa kuwa mwangalifu zaidi kwa watoto wako ili kuwaepusha ma madhara yanayoweza kuepukika.

Mbali ya baba na mama kuathiriwa na matumizi ya simu kundi jingine ni la  watoto kuanzia umri wa miaka 7 na kuendelea. Umri huo ndio unauhitaji mkubwa wa kuwa karibu na wazazi kwa sababu watoto huanza tabia ya kuiga mambo mbalimbali yakiwamo mabaya.

Si vyema mzazi kurudi nyumbani na kuikumbatia simu zaidi badala ya kufuatilia maendeleo ya watoto na kuwachunguza mienendo yao kitabia.

Hali hii inaweza kuchangia kushindwa kujua mahudhurio ya mtoto wako hata kama haendi shule huwezi kujua.

Wazazi wanapaswa kuwa makini katika matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuangalia muda na sehemu mliyopo.

Kama unaona huwezi kukaa bila kuchati ni vema ukifika nyumbani uanze kuzima data kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yako kama mzazi.

Hii itakusaidia kuwa utaratibu mzuri wa kuangalia maendeleo ya watoto wenu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles