24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Sirro: Kagera itanufaika fedha za ujenzi wa nyumba za polisi

Na Renatha Kipaka -Bukoba


MKUU wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, amesema Kagera itakuwa miongoni mwa mikoa 10 itakayonufaika na Sh bilioni 10 zilizotolewa na Rais Dk. John Magufuli.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana wakati akihitimisha ziara yake mkoani Kagera.

Sirro alisema jeshi hilo linatarajia kukabidhiwa Sh bilioni tatu na laki saba zitakazotumika kujenga nyumba 10 katika mikoa tofauti.

Alisema Sh bilioni sita na laki tatu zitakazotolewa awamu ya pili zitatumika kujenga nyumba katika mikoa mingine ikiwamo Kagera.

Katika hatua nyingine, alisema amezungumza na IGP wa nchini Rwanda kuhusu suala la ujangili.

Sirro alisema kumekuwapo na malalamiko ya baadhi ya Watanzania kufanya ujangili katika mbuga nchini Rwanda na Wanyarwanda kufanya vitendo hivyo katika mbuga za Tanzania.

Alisema wamekubaliana kuwa askari wa pande zote mbili watakutana na wananchi wanaozunguka Mto Kagera kuwakumbusha umuhimu wa kutii sheria ili kukomesha vitendo vya ujangili.

Pia amelitaka jeshi hilo kuwachukulia hatua na kuwaelimisha wananchi wanaojihusisha na biashara ya magendo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles