27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Siri ya Prince Jack Bushiri yavuja

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KATIKA kuadhimisha mwaka mmoja wa kuzaliwa kwa mtoto wa mdau mkubwa wa muziki nchini Marekani, Bushiri Dems anayeitwa Prince Jack Bushiri, siri ya ujio wake kwenye familia hiyo imevuja.

Akizungumza na Mtanzania Digital jana Bushiri Dems, amesema mwaka 2020 ulikuwa mchungu kwa familia yao kwani walipotelewa na kaka yao anayeitwa Jack, nchini Tanzania ambaye mpaka leo hajaonekana lakini Mungu aliwapa zawadi ya mtoto Prince Jack Bushiri aliyezaliwa Desemba 19, mwaka jana ikiwa ni miezi miwili baada ya ndugu yao kutoweka.

“Mwanangu Prince Jack Bushiri amegomboa mtu aliyepotea maana baada ya kaka kupotea huko Tanzania alizaliwa yeye na amekuwa mtu muhimu kwetu maana alirejesha furaha iliyopotea kwenye familia, tunamshukuru Mungu kwani leo mwanangu anatimiza mwaka mmoja wa kuzaliwa kwake, ingawa kaka hajapatikana mpaka sasa lakini Prince Jack Bushiri amekuwa faraja kwetu,” amesema Bushiri ambaye ni bosi wa lebo ya Dems International inayowasimamia wasanii wengi wa Afrika wanaoishi Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles