23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Siri nzito ndege za Urusi, China kuvamia Korea Kusini

MOSCOW, URUSI

URUSI imekana kuiomba msamaha Korea Kusini  kutokana na  ndege zake kudaiwa kuingia katika anga lake, huku mazoezi ya  ndege  za kivita kutoka katika mataifa manne yakielezwa kuendelea eneo hilo.

Ndege hizo zikiwemo za Urusi na China zinafanya mazoezi katika visiwa vyenye mgogoro vya Dokdo/Takeshima ambavyo vinagombaniwa na Korea Kusini na Japan.

Awali Ofisi ya Rais ya Korea Kusini ilitoa taarifa ikieleza kuwa Urusi ilieleza kusikitishwa na tukio hilo na hivyo kuomba msamaha.

Ofisi hiyo ya rais ya Korea Kusini ilieleza kuwa Urusi ilisema sababu ya tukio hilo ni tatizo la kiufundi.

Msemaji wa Ofisi hiyo ya rais, Yoon Do Han aliwaambia waandishi wa habari kuwa Urusi  kupitia jeshi imesema wizara yake ya ulinzi itaanzisha uchunguzi mara moja na itachukua hatua zinazostahili.

Hata hivyo Urusi jana ilikana kutoa ujumbe  huo ikisisitiza kuwa  haikuingia katika anga la taifa jingine na zaidi ilieleza kuwa kuna mengi kuhusu hilo na Korea Kusini  bado haijajibu ukweli.

“Tumeona tamko kwenye vyombo vya habari vya Korea Kusini vikikariri maneno yanayodaiwa kuzungumzwa na mwakilishi wetu wa ubalozi wa

kijeshi,”  Msemaji wa Ubalozi wa Urusi nchini Korea Kusini alisema.

“Tunafuatilia kwa makini matamko haya, na katika hili tunaweza kujisemea wenyewe kwamba kuna mengi ndani yao ambayo hayalingani na hali halisi na kile ilichozungumza.”

Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisisitiza kuwa  ndege zake na zile za China zilipiga doria ya angani kwa pamoja kwa mara ya kwanza.

Tukio hilo lilizilazimisha ndege za Korea Kusini kurusha takribani risasi 400 za onyo na milipuko 20 karibu na ndege ya kijasusi ya Urusi  iliyokuwa ikiruka karibu na visiwa hivyo vyenye mgogoro vilivyoko katika bahari ya Japan inayojulikana pia kama Bahari ya Mashariki.

Tukio hilo ambalo lilianza Jumanne, Japan nayo ilijibu kwa kurusha mabomu.

Wakati huo huo China imetetea zoezi hilo la doria ya pamoja  ya anga kwa mara ya kwanza kati yake na Urusi .

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa China, Wu Qian  aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanafuata taratibu na sheria za kimataifa na hawakuingia katika anga la nchi nyingine.

Korea Kusini inasema doria hiyo ilifanyika bila ilani jambo lililosababisha kutoa onyo kwa kufyatua risasi kupitia ndege zake za kivita.

Jeshi la Korea Kusini lilisema jumla ya ndege tatu za Urusi na mbili za jeshi la China ziliingia katika anga lake la kijeshi ‘Korea Air Defence Identification Zone’ (KADIZ) Jumanne asubuhi.

Miongoni mwa ndege hizo ni ile ya A-50  ya kijasusi ya Urusi – ambayo iliingia kinyume katika eneo lake mara mbili kabla ya kuondoka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles