27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Boris Johnson atangaza vipaumbele vyake

LONDON, UINGEREZA

WAZIRI Mkuu mpya wa Uingereza, Boris Johnson ameainisha mambo kadhaa ambayo yatatekelezwa na serikali yake mpya.

Johnson ambaye alikuwa akizungumza katika makazi ya Malkia baada ya kujadiliana naye kuhusu serikali yake aliyataja baadhi ya mambo hayo ni pamoja na suala la zima la Brexit ambalo alisemea litatekelezwa Oktoba 31.

Zaidi alivitaja vipaumbele vyake kuwa ni kushughulikia masuala ya ndani ikiwa ni pamoja na huduma za kijamii na idadi ya polisi.

Awali akikabidhi rasmi nafasi hiyo, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza aliyetangaza kujiuzulu Theresa May katika hotuba yake aliitakia mema serikali ya Johnson, na kuongeza: “mafanikio yao yatakuwa ni ya nchi yetu,”.

Alisema kuhudumu kama Waziri Mkuu lilikuwa ni jambo la heshima kubwa na aliwashukuru watu wote aliofanya nao kazi.

” Hii ni nchi yenye malengo na fursa, na nina tumaini kila msichana mdogo ambaye amemwona Waziri Mkuu mwanamke sasa anatambua kwamba hakuna cha kuzuia kile ambacho anataka kufanikisha.”

May alisema ataendelea na nafasi yake ya ubunge na alikuwa akitarajia naye kuuliza maswali katika siku zijazo.

Alisema anafuraha kukabidhi kwa mrithi wake suala la Brexit ili kulifanikisha kwa ajili ya maslahi ya nchi hiyo.

Wakati May akizungumza  alikatishwa na sauti ya waandamanaji waliotamka “acha Brexit!” lakini alijibu akisema: “nafikiri jibu la hilo ni – nafikiri siyo.”

Awali wakati akikabidhi mikoba kwa Waziri Mkuu mpya, May alikabiliwa na maswali kwa mara ya mwisho na alionekana dhahiri kukasirishwa.

Kiongozi wa Labour, Jeremy Corbyn  akimzungumzia May alisema anaheshimika kwa jamii lakini alimkosoa kweny rekodi za uchumi, watu wasio na makazi na Brexit.

Katika majibu yake kuhusu hilo, aliorodhesha yale aliyoona kama ni mafanikio yaliyoletwa na uongozi wake ambayo ni kuimarisha shule kuongeza ajira na kuongeza namba ya watu kumiliki makazi.

Awali wakati akielekea kwenye mwaliko wa Malkia kwa ajili ya kuunda serikali, gari ya Johnson ilivamiwa na waandamanaji kutoka Greenpeace.

Johnson ambaye ni meya wa zamani wa London ameshika nafasi hiyo baada ya kupata ushindi mkubwa wa asilimia 66.4 ya kura zote dhidi ya Waziri wa mambo ya Nje wa Uingereza, Jeremy Hunt.

Taarifa zinaeleza kuwa kulikuwa na mazungumzo kati ya Johnson na Hunt juu ya Waziri wa Mambo ya Nje ambaye ataongoza katika utawala wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles