23.6 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

SIR GEORGE KAHAMA AFARIKI DUNIA

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM


MMOJA  wa waasisi wa Uhuru na aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Tanganyika, Sir George Kahama (88), alifariki dunia Dar es Salaam jana.

Akithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Stephen, alisema Sir Kahama alipatwa na  mauti jana saa 4:40 jioni.

Alisema Sir Kahama alifikishwa hospitalini hapo akiwa katika hali isiyoridhisha na kupokewa katika chumba cha uchunguzi kwa ajili ya matibabu.

MTANZANIA ilipomuuliza ugonjwa uliokuwa ukimsumbua, John alisema kwa suala hilo linaweza kuzungumziwa na familia na si yeye.

“Tulimpokea hapa hospitali Ijumaa, hakuwa  katika hali nzuri  ya afya na aliingizwa katika chumba cha uchunguzi na  kupatiwa matibabu lakini leo (jana) saa 10.00 jioni aliaga dunia ,’’alisema John.

 Kahama maarufu kama Sir George Kahama  alizaliwa Novemba 30, 1929  na aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani (1961-1962) kabla nafasi hiyo haijachukuliwa na  Oscar Kambona  kwa mwaka mmoja kuanzia mwaka 1962 hadi 1963.

 Sir Kahama ambaye alizaliwa Novemba 30, 1929 aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani (1961-1962) kabla nafasi hiyo haijachukuliwa na  Oscar Kambona  kwa mwaka mmoja kuanzia mwaka 1962 hadi 1963.

Alikuwa mtumishi wa umma kwa miaka mingi  na mwanasiasa   mahiri na makini, katika utendaji kazi kuanzia nyakati za Tanganyika za kudai uhuru katika  miaka ya 1950 hadi kujitawala mwaka 1961.

Mwanasiasa huyo   alipelekwa   Uingereza na Chama cha Ushirika wa   Kahawa cha jimbo lililokuwa likiitwa Ziwa Magharibi wakati huo, likiwa la Wilaya za Bukoba, Karagwe, Biharamulo na Ngara.  Kwa sasa ni Mkoa wa Kagera.

Katika kutimiza dhana yao ya kuzima harakati za Nyerere za kudai uhuru na kwa vile hakuwa peke yake katika harakati hizo, wakoloni walimpatia masurufu yasiyokidhi mahitaji yake akiwa masomoni ili akose uwezo wa kuwasiliana na waasisi wenzake.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya wanachuo wenzake kutoka Tanganyika   katika vyuo mbalimbali vya Uingereza walidokezwa uwepo wake nchini humo.

  Mwalimu Nyerere alifurahi akawa na matumaini ya kusaidiwa, kwanza kwa sababu alikwisha kuona ushirikiano wa Watanganyika wengine hivyo akajua hata Kahama atamsaidia.

Kwa mujibu wa Sir George, katika moja ya mahojiano yake kabla ya kupatwa na mauti, alisema tumaini la Mwalimu Nyerere wakati huo lilizidishwa na ukweli kwambawao ni watani wa jadi.

 Sir George aliingizwa kimyakimya katika harakati za kudai uhuru wa iliyokuwa Tanganyika.

Alikuwa rafiki wa karibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu  Nyerere,   chanzo cha urafiki wao likiwa ni  jibu la jinsi gani   alivyoingizwa kwa siri katika siasa za Tanganyika.

  Nyerere na Kahama waliporejea nchini kila mmoja aliripoti kwa mwajiri wake, huku  Mwalimu Nyerere akilazimika kujiuzulu kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari Pugu, Dar es Salaam   kusudi aendeleze kwa ukamilifu siasa za kudai uhuru.

Naye  Kahama aliendelea na kazi katika chama cha ushirika wa zao la Kahawa jimboni Ziwa Magharibi (BCU) mjini Bukoba.

Wakati inaundwa Serikali baada ya Uhuru, ndipo Mwalimu Nyerere alipomwita Sir George kutoka Bukoba  ajiunge na Baraza la Mawaziri la Serikali hiyo  na akamteua kuwa Waziri wa Ushirika na Masoko na mwenyewe (Nyerere) akawa Waziri Mkuu.

Baadhi ya mawaziri walioteuliwa walikuwa Paul Bomani, Chifu Abdallah Fundikira, Rashid Mfaume Kawawa, Solomon Eliofoo, Nsilo Swai, Said Maswanya, Dereck Noel Bryceson, Sir. Ernest Versey na Amir Jamal.

Sir. George alikuwa Waziri wa kwanza wa Mambo ya Ndani ya Nchi na baadaye Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alimteua tena kuwa Waziri wa Ushirika.

JPM amlilia

Rais Dk. John Magufuli, ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mmoja wa Waasisi wa Taifa na Waziri Mstaafu, Sir George Kahama.  

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilieleza kwamba   Dk. Magufuli, alisema Taifa limempoteza mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru, maendeleo na ustawi wa jamii ya watanzania akiwa katika nyadhifa mbalimbali za uongozi hususan kuwa miongoni mwa mawaziri katika Baraza la kwanza la Mawaziri.

“Sir George Kahama alikuwa kiongozi shupavu, mzalendo, mwanasiasa mahiri, aliyewapenda Watanzania na aliyejitoa kushirikiana na viongozi wenzake akiwamo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere kupigania uhuru, kujenga misingi ya Taifa likiwamo Azimio la Arusha, kujenga misingi ya uchumi wa ujamaa na kujitegemea na mengine mengi.  Kwa hakika hatutamsahau,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles