29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Singida Bisg Stars yapigwa bei, sasa kuitwa Singida Fountain Gate Fc

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Timu ya Singida Big Stars imetangazwa kuuzwa na sasa itakuwa inamilikiwa kwa asilimia 100 na Mkurugenzi wa Shule za Fountain Gate, Japhet Makau.

Akizungumza Dar es Salaam leo Juni 14 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Bosi huyo mpya wa Singida amesema kuwa lengo la kununua timu hiyo ni kukuza vipaji vya wachezaji na kutimiza ndoto zao kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mashindano mengine ya kimataifa.

Amesema Timu ya Singida Big Stars baada ya kuuzwa imabadilisha jina kwa sasa itakuwa inaitwa Singida Fountain Gate Fc.

“Timu ya Singida Big Stars tumeuuziwa kwa sharti kubwa moja ambalo lazima timu makazi yake yawe Singida ndiyo makubaliano hayo na timu kuwa Singida hakuna tatizo kwa sababu historia ya timu imeanzia huko,” amesema Makau.

Amesema ndoto yao kubwa ili kuwa ni kuja kumiliki timu kubwa nchini na watahakikisha timu hiyo inaendelea kufanya vizuri kama ilivyokuwa awali.

Makau amesema timu hiyo itakuwa na Bodi ya Wajumbe tisa ambapo baadhi yao ni John Kadutu, Festo Sanga(Mbunge wa Makete), Joseph Msafiri, Ibrahim Mirambo, Mussa Sima na wengine.

Aidha, amesema mazungumzo yanaendelea kuwepo jinsi ya kuendeleza timu hiyo na watahakikisha inakuwa timu bora.

Naye aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Timu ya Singida big stars amesema kuwa kwa mwaka mmoja wamekuwa kwenye ligi kuu
wamepata mafanikio makubwa.

“Lengo kubwa la timu hiyo ni kushiriki ligi kuu na walifanya uwekezaji mkubwa kwa msimu huu ulioisha na timu imeingia “Top Four” na itashiriki mashindano ya kimataifa tumetimiza malengo tayari kazi kwa mwekezaji mpya,” amesema Kadutu.

Amesema mchezo wa mpira ni ajira na unakuza vipaji kwa vijana na unachangia kukuza uchumi wa nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles