25.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Shauritanga na mkakati wa kuzalisha wasomi nchini

Na Safina Sarwatt, Rombo

Sekta ya Elimu na Mafunzo, kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 na Mpango wa muda mrefu wa Maendeleo ya Taifa 2011/12 hadi 2024/25, inatarajiwa kuleta Maendeleo ya haraka ya rasilimali watu kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya Watanzania walioelimika.

Makamu mkuu wa shule Sekondari Shauritanga.

Sambamba na hilo, mfumo huu unawajibika kutoa elimu na mafunzo yenye ubora unaokubalika na kutambulika Kitaifa, Kikanda na Kimataifa.

Hata hivyo, katika kipindi hicho, changamoto mbalimbali zimejitokeza zikiwemo udhaifu
katika mfumo wa elimu na mafunzo, uhaba wa walimu, uhaba wa zana, nyenzo na vifaa na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na udhibiti.

Katika kufikia malengo makubwa ili kuzalisha watalamu bora watakaoweza kuendana na ushindani wa soko la ajira nchini, Shule ya Sekondari ya Shauritanga iliyoko Rombo Mashati inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imejizatiti kuhakisha inazalisha watalamu bora na waadilifu kwa maslahi mapana ya Taifa.

Even Deogratius mwanafunzi kidato cha sita mwaka 2019.

Shauritanga ni miongoni mwa shule zinaendelea kufanya vizuri katika kutoa elimu inayoendana na mabadiliko ya soko la ajira ya ndani nje ya nchi.

Mafaniko hayo yanatokana na ubunifu mkubwa wa walimu na wasimamizi wa shule hiyo kuendelea kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za elimu ikiwemo miundombinu bora ya shule, vifaa vya kufundishia.

Akielezea mafaniko hayo mkuu wa shule hiyo Ally Mgaya amesema walimu wamekuwa wakishirikiana na wazazi kuhakikisha wanafunzi wapata elimu bora pamoja maadili mema ya Kitanzania.

Amesema kuwa walimu wamekuwa na upendo na kuwawazale na kuangaliza maslahi ya taifa lengo kubwa nikuunga mkono juhudi ya Serikali katika hakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora bila ubaguzi wa aina yoyote ile.

Amesema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita.

Ameongeza kuwa shule imejikita zaidi katika masomo mbalimbali hususan sayansi lengo ni kuzalisha watalamu wengine zaidi ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu sayansi na madaktari katika hospitali zetu hapa nchini.

Aidha, licha shule kufundisha masomo yote kipaumbe kubwa ni sayansi ili kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya viwanda na afya ambapo kunauhitaji mkubwa.

“Serikali ya sasa ni ya uchumi wa viwanda na tumeona Rais Dk. Samia Suluhu ameendelea kufungua milango kwa wawezaji kuwekeza viwanda hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kusimama katika nafasi yake kuhakikisha tunasimama na mama.

“Shule ina walimu wenye sifa na mahiri katika ufundishaji na mazingira bora na rafiki kwa ajili ya kujifunzia, ambapo masomo yanayofundishwa ni pamoja CBG,PCB,PGM,EGM,HGE,HGL,HGK,PCM,” amesema.

Amesema shule hiyo pia ina nafasi chache kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza, tatu, nne na kidato cha sita .

Nao baadhi ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita shule hapo wanaeleza siri ya mafaniko yao huku wakishukuru uongozi wa shule kwa malezi mazuri.

Wamesema kuwa siri kubwa ufaulu ni malezi mazuri ya walimu pamoja na maombi na kusoma kwa bidii kama tunavyoelekezwa na walimu wetu.

“Tuna mengi ya kueleza kuhusu shule hii walimu walikua na upendo sana walitulea kama watoto wao pia walitusihi sana suala nidhamu na kumheshimu kila mtu hayo ndiyo siri kubwa ya mafaniko mnayoyaona leo,”amesema mmoja wa Wanafunzi hao.

Mwanafunzi mwingine anayefahamika kama, Even Deogratius, amesema amehitimu kidato cha sita mwaka 2019 na kwamba amepata elimu bora inayomwezesha kukabiliana na ushindani wa soko la ajira.

“Kuna dhana potofu ambayo imejengeka kwa baadhi ya watu kwamba ni shule ya chama, lakini nataka niwambie kwamba elimu haina chama badala yake walete watoto,” amesema.

Shule hiyo ambayo ni ya kutwa na bweni pia inalelewa na kanisa katoliki wanafunzi wamekuwa wakifundishwa suala la imani na maadili mema ya kitanzania.

Makamu mkuu wa shule hiyo, Melisa Kawiche amesema kuwa wamekuwa wakiwafundisha wanafunzi suala uzalendo na kujiamini kwani ndiyo sila kubwa ya mafanikio katika maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles