29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Watengeneza batiki wageukia masoko ya kimataifa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wanawake wanaojihusha na utengenezaji batiki mkoani Dar es Salaam wamemuomba Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuwasadia kuwaunganisha na fursa katika masoko ya kimataifa.

Wanawake watengeneza batiki katika Soko la Mchikichini, Dar es Salaam.

Wakizungumza Juni 14, 2023 wakati wa mafunzo kuhusu mitaji na fursa za mikopo wanawake hao wamesema changamoto kubwa inayowakabili ni soko la kueleweka la bidhaa za batiki hasa nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake Watengeneza Batiki Soko la Mchikichini wilayani Ilala (KIKUWASO), Elinaike Kimathi, amesema wanajitahidi kutengeneza bidhaa bora lakini bado hazifikiwi kikamilifu na wateja hivyo kushindwa kupata kipato cha kuridhisha.

“Hivi sasa kuna soko la kimataifa la Afrika Mashariki, sisi wanawake watengeneza batiki hatuna mtu wa kutushika mkono. Tunamwomba Rais Dk. Samia atusaidie,” amesema Elinaike.

Pia wameiomba Serikali kulegeza masharti ya mikopo inayotolewa na halmashauri kwa sababu vikundi hivyo vimekuwa vikishindwa kukopesheka kutokana na wanachama wake kutoka katika maeneo tofauti.

“Tangu mikopo ianze kutolewa sisi hatujanufaika nayo kwa sababu halmashauri wanasema tunatoka katika maeneo tofauti,” amesema.

Naye Katibu wa KIKUWASO, Adela Swai, amewaomba wauzaji wa malighafi za batiki kupunguza gharama ili waweze kuongeza ufanisi kwani hivi sasa gharama ni kubwa.

Kwa upande wa Eunice Tugala, ambaye ni mtengenezaji batiki kutoka Msasani Wilaya ya Kinondoni, ameiomba serikali kuwashirikisha katika maonyesho ya kimataifa.

Akitoa elimu ya akiba na mikopo, Ofisa Uhusiano wa Benki ya Azania, Abishua Mganga, amesema kwa kutambua changamoto ya mitaji kwa wajasiriamali wameanzisha akaunti maalumu ya ‘Mwanamke Hodari’.

Amesema mjasiriamali anapokuwa na akaunti hiyo anaweza kukopa hadi mara nne ya akiba aliyoiweka hadi Sh milioni 500 na kuwataka wanawake hao kuchangamkia fursa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles