25.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 28, 2024

Contact us: [email protected]

CHAMATA chawaangukia Wakuu wa Wilaya nchini

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Chama Cha Maafisa Afya Tanzania-(CHAMATA) kimeomba Wakuu wa Wilaya na Viongozi wengine wa Serikali kuwaunga mkono pindi wanapotekeleza majukumu yao kwani majukumu yao ni magumu na wanafanyakazi na watu wasio wahitaji.

Wito huo umetolewa Juni 14, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Mubarak Twaha, ambapo amesema lengo la maafisa afya ni kulinda Afya ya Jamii na Mazingira.

“Kumekuwepo na wakuu wa wilaya kukamata maafisa afya wakati wakitimiza majukumu yao, mfano Mkuu wa Wilaya Kinondoni alitoa amri Afisa Afya akamwatwe tukio hilo lilitokea Mei 22, mwaka huu kata ya Kijitonyama wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru viongozi walifatilia walikuta hana kosa, hivyo viongozi wanakuja na maamuzi bila kutupa nafasi ya kuongea na viongozi,” amesema Twaha.

Amesema viongozi wanapaswa kutoa nafasi ya kufanya kazi, kutengenezewa mazingira bora ya kazi na kwamba haki ya kutunza mazingira ni kazi yao na kuelimisha jamii.

Amesema kuendelea kuwaweka ndani maafisa afya ni kuwatengenezea mazingira magumu ya kazi kwa wananchi na viongozi na kwamba wanawakatisha tamaa maafisa hao.

Aidha, amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa kutekeleza majukumu hawapati nafasi ya kuzungumza na viongozi ili kujua wanayopitia.

Twaha amesema hawawezi kulea mtu anayefanya kazi kinyume na sheria nakwamba atashughulikiwa na vyombo husika huku akisisitiza kuwa wajibu wao ni kulinda jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles