25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yaibomoa JKT Tanzania ikiisubiri Yanga Oktoba 18

 ASHA KIGUNDULA – DODOMA 

SIMBA imeendeleza ubabe wake katika LigI Kuu Tanzania Bara msimu huu, baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji wao JKT Tanzania, mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma. 

Simba iliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kuandika bao la kwanza dakika ya tatu kupitia kwa Meddie Kagere. 

Kagere alifunga bao hilo kwa kichwa akimalizia pasi ndefu ya kiungo Larry Bwalya. 

Bao hilo liliongeza morali ya wachezaji wa Simba kwani dakika ya tano, mshambuliaji Chris Mugalu aliifungia bao la pili akiunganisha pasi ya Luis Miquisson. 

Dakika ya 35, mchezaji wa JKT Tanzania, Richard Maranya alionyeshwa kwa kadi ya njano, baada ya kumkwatua Jonas Mkude. 

Kabla ya timu hizo kwenda mapumziko, Kagere aliifungia Simba bao la tatu dakika ya 40 kwa shuti la mguu wa kushoto, ikiwa ni baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Bwalya, Clatous Chama na Miquissone. 

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikamilika Simba ikiwa mbele kwa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania. 

Kwa ujumla kipindi cha kwanza, Simba iliutawala mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa JKT. 

Kipindi cha pili, Simba iliingia uwanjani na mpango kazi ule ule wa kushambulia kwa kasi. 

Dakika ya 53, Miquisson aliifungia Simba bao la nne kwa mkwaju wa mbali. 

Dakika ya 50, kipa wa JKT Tanzania, Patrick Muntari alionyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Miquissone

 Dakika ya 59, alitoka Kagere kwa upande wa Simba na kuingia Muzamiru Yasin. 

Dakika ya 72, Pascal Wawa alionyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Mohamed Nurdin. 

JKT Iilifanya mabadiliko dakika ya 58, alitoka Maranya na nafasi yake kuchukuliwa na Danny Lyanga kabla ya dakika ya 61 kutoka Mugandila Shaban nafasi yake kuchukuliwa na Kelvin Nashon. 

Dakika ya 73, alitoka Chama na nafasi yake kuchukuliwa na Bernard Morrison kabla ya Miquissone kutoka na kuingia Hassan Dilunga. 

Dakika 90 zilikamilika kwa Simba kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT. 

Katika mchezo mwingine, Biashara United iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Karume Musoma. 

Kikosi cha JKT Tanzania: Patrick 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles