25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Rooney ampigia ‘debe’ Harry Kane

 LONDON, ENGLAND 

NYOTA wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, ameutaka uongozi wa timu hiyo kuhakikisha unainasa saini ya mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane badala ya Jadon Sancho wa Borussia Dortmund. 

Dirisha la usajili barani Ulaya linatarajiwa kufungwa usiku wa kuamkia kesho, hivyo klabu mbalimbali zinapambana kuhakikisha zinakamilisha sajili zao kabla ya saa 5:59, usiku. 

Manchester United msimu huu wamekuwa wakihusishwa na mshambuliaji huyo wa pembeni wa Dortmund, lakini hadi sasa dili hilo linaonekana kuwa ngumu kutokana na uongozi wa Dortmund kuhitaji kiasi cha pauni milioni 108, jambo ambalo United wanadai kuwa kiasi hicho cha fedha ni kikubwa. 

Rooney amedai United ni bora wakawekeza fedha zao kwa Kane ambaye alimuachia kitambaa cha unahodha wa timu ya taifa England tangu mwaka 2018, kuliko kuangaika na Sancho. 

Kwa upande mwingine Rooney anaamini kukamilisha dili hilo la Kane litakuwa ngumu kwa kuwa Tottenham hawapo tayari kuachana na mshambuliaji huyo. 

“Jadon Sancho ni mchezaji bora kwa sasa na amekuwa mmoja kati ya wachezaji ambao wanawindwa na Manchester United wakati huu wa kiangazi, lakini nashangaa kwa nini watu wanaangaika na mchezaji ambaye anatajwa kuwa na thamani ya kuanzia pauni milioni 100, wakati wapo wenye uwezo kama wake na thamani yao ipo chini? 

“Manchester United wana wachezaji kama vile Marcus Rashford na Anthony Martial, itakuaje endapo watafanikiwa kumsajili Sancho huku wana mchezaji kama vile Mason Greenwood ambaye anacheza nafasi moja na mchezaji huyo na hata umri wanalingana? Hivyo kwa upande wangu ni bora kiasi hicho cha fedha wakiweke mezani ili kumsajili Harry Kane. 

“Ndio, najua kumtoa Kane ndani ya Tottenham ni ngumu, lakini Manchester United ni miongoni mwa klabu ambazo zinaweza kuingia sokoni na kumsajili mchezaji bora na Kane ni kati ya wachezaji ambao wanafaa kucheza United chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer, wachezaji wengine ni kama vile Erling Haaland ambaye walishindwa kuinasa saini yake msimu uliopita,” alisema Rooney. 

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles