30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yaibadilishia kikosi Singida

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kuelekea mechi yao na Singida Fountain Gate, Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kutokana na kucheza mechi kila baada ya siku mbili watakuwa na mabadiliko katika kikosi chao kwani baadhi ya wachezaji wamepewa mapumziko.

Matola amesema hayo leo Machi 11,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

“Kwa sababu ukingali ‘game’ zipo kila baada ya siku mbili kwa hiyo nafikiri  kunaweza kuwa na mabadiliko kutokana na kuwapa baadhi ya wachezaji mapumziko, sisi kama benchi la ufundi tutaangalia ni nani anaweza kutufaa katika mchezo wa kesho,” amesema Matola.

Aidha amesema morali yao ipo juu na bado wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika ligi kuu na kuahidi kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo.

Amekiri kuwa walifanya makosa katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Tanzania Prisons Coastal Union  kwa kuruhusu mabao lakini wameshajirekebisha mazoezini.

Katika mchezo uliopita Wekundu wa Msimbazi hao waliifunga Coastal Union 2-1 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles