31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Gamondi, kipa Coastal Union watwaa tuzo

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amechaguliwa kuwa kocha bora wa Februari na kutwa tuzo ya TFF, akiwashinda kocha wa Simba Abdelhak Benchikha na Ahmad Ally wa Tanzania Prisons.

Gamondi ameibuka kededea kutokana na kuiongoza Yanga katika michezo mitano bila kupoteza, akishinda minne na sare moja.

Michezo iliyompa tuzo kocha huyo ni sare ya 0-0 na Kagera Sugar, amezifunga Dodoma Jiji 1-0, Mashujaa 2-1, Prisons 1-2 na KMC 0-3.

Naye Kipa wa timu ya Coastal Union, Ley Matampi ametwaa tuzo ya Februari ya mchezaji bora wa mwezi baada ya dakika 270 za michezo mitatu bila kuruhush bao.

Kipa huyo amewashinda kiungo wa Yanga Mudathir Yahya na mshambuliaji wa Prisons Samson Mbangula aliongia nao fainali.

Pia kamati ya tuzo hizo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Azam Complex, Amir Juma kuwa meneja bora wa mwezi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles