22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

SILAHA 37 ZA MOTO ZAKAMATWA MKOANI TANGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kukamata silaha za moto 37 ambazo zilikuwa zikitumika katika matukio ya uhalifu mkoani hapa.

Pamoja na hili jeshi hilo pia limekamata risasi 474 ambapo kati ya hizo risasi 425 zilikuwa za SMG, 24 zilikuwa za Shotgun huku 25 zikiwa za Rifle.

Akitoa taarifa ya hali ya usalama mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema kwa kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka huu wamefanikiwa kuzima matukio ya uhalifu pamoja na kusambaratisha mitandao ya aina hiyo.

Alisema kwa kipindi hicho wamefanikiwa kukamata siala aina SMG nane, Marker IV mbili, Shotgun nne, Pistol moja  na Rifle mbili ambazo zilikamatwa kwenye matukio mbalimbali mkoani hapa.

Alisema katika ya silaha hizo pia mabomu manne ya kurusha kwa mkono na Gobore 20 zilikamatwa kwa watuhumiwa wa uhalifu ambayo yalikuwa yakitumika kufanyia vitendo viovu.

“Vilevile katika kipindi hicho tuliweza kukamata risasi 425 za SMG, risasi 24 za Shotgun na risasi 25 za Rifle zilizokamatwa kutokana na misako mbalimbali iliyofanywa na Jeshi la Polisi kwenye matukio mbalimbali,” alisema RPC Wakulyamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles