25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

WAKAZI WA MBEZI WASAKA MATAPELI WA ARDHI

William Lukuvi
William Lukuvi

Na MWANDISHI WETU-Dar es  Salaam

WAKAZI wa Mtaa wa Kilongawima eneo la Mbezi, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wameanza kuwasaka watu wanaodaiwa kuuza viwanja vyao kinyume cha taratibu.

Msako huo umeanza mapema mwezi huu baada ya kutokea mapambano baina ya wakazi wa mtaa huo na kundi la watu lililovamia na kuvunja baadhi ya nyumba zao kwa maelezo ya kutekeleza maagizo ya wamiliki halali wa viwanja hivyo.

Wakizungumza na gazeti hili mapema wiki hii katika ofisi za Serikali ya Mtaa ya Kilongawima, walisema wameamua kuanza operesheni ya kupambana na matapeli wa viwanja wanaouza maeneo yao kinyume cha taratibu.

Walisema wameanza msako huo kwa kuwatafuta washirika wa matapeli wa viwanja waliodai kuwa wanaishi miongoni mwa jamii yao.

Mmoja wa walalamikaji aliyejitambulisha kwa jina la Charles Mwanga, alilieleza gazeti hili kuwa yeye ni mkazi wa eneo la Mbezi Block L, Mtaa wa Kilongawima ambaye nyumba yake ilibomolewa na kundi la watu waliokodiwa na matapeli kabla ya kutimuliwa na wananchi.

“Tumeamua kuunganisha nguvu kuwasaka watu wanaotumia nyaraka za bandia kuuza maeneo yetu kwa matajiri ambao huwadanganya kuwa wao ndiyo wamiliki halali wa viwanja vyetu.

“Hawa watu ni hatari, ni matapeli wa kimataifa kwa sababu wanatengeneza nyaraka za bandia zinazoonyesha wao ndiyo wamiliki wa maeneo yetu kisha wanatafuta watu wenye fedha wanawauzia. Na tumebaini wanashirikiana na baadhi ya wenzetu tunaoishi nao.

“Mimi walikodisha watu kuja kuvunja nyumba yangu mwezi uliopita kabla ya wananchi hawajachachamaa na kuwatimua. Sasa tumeanza kuwasaka ili tuwakabidhi kwenye vyombo vya sheria,” alisema Mwanga.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilongawima, Paulo Richard  alipoulizwa kuhusu uvamizi na kubomolewa kwa nyumba za baadhi ya wakazi wa eneo analoliongoza alisema ni kweli kumekuwa na matukio mengi ya aina hiyo ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wa eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles