24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Shuwasa yadai milioni 949/- taasisi za jeshi

Na DAMIAN MASYENENE  – SHINYANGA

MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga (Shuwasa) inazidai taasisi za jeshi mkoani hapa jumla ya Sh 949,111,561 ambazo ni malimbikizo ya madeni ya ankara za mwisho wa mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2016 hadi 2019.

Taasisi hizo zinazodaiwa madeni hayo ni Jeshi la Wananchi (JWTZ) Sh 520,244,975, Magereza Sh 252,520,120 na Jeshi la Polisi Sh 127,349,465, huku ikielezwa kuwa jitihada za kuhakikisha madeni hayo yanalipwa zimeshindwa kuzaa matunda.

Hayo yameelezwa jana mjini Shinyanga na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shuwasa, Deogratias Sula wakati wa hafla fupi ya kuzindua bodi mpya.

Alimwomba Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa aweze kufanya mazungumzo na wizara zinazozisimamia taasisi hizo ili madeni hayo yalipwe.

“Katika kipindi chetu cha miaka mitatu tumetatua changamoto nyingi, lakini tumebakiwa na chache ambazo ni sugu, kubwa kabisa ni taasisi za Serikali kusuasua katika kulipia madeni ya ankara za maji za mwisho wa mwezi na hadi Novemba, 2019 jitihada za kufuatilia madeni hayo hazijazaa matunda,” alisema Sula. 

Akijibu hoja hizo, Mbarawa alisema Serikali inalitambua deni hilo na kwamba wamesikia kilio cha mamlaka hiyo, hivyo kuwaomba wawape muda kulishughulikia na kuwaahidi kuwa litalipwa.

“Tumewasikia, tunalifahamu na taratibu zimeanza kufanyika, litalipwa na tunawasisitizia mfunge mita za pre-paid ili kudhibiti matumzi ya maji,” alisema Mbarawa.

Awali akiwasilisha taarifa ya shughuli za Shuwasa, Mkurugenzi Mtendaji wa Shuwasa, Flaviana Kifizi, alisema kwa sasa wanao wateja 21,505 na wanatarajia kufikia 25,000 ifikapo mwaka 2021 na kuongeza mtandao wa maji kufikia kilometa 20 katika kilometa 549.12 za sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles