23 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Mtuhumiwa alalamika upelelezi shtaka

NA KULWA MZEE -DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeendesha kesi kwa njia ya video huku mshtakiwa, Baraka Mkuki akiwa katika Gereza la Keko akilalamikia upelelezi wa shauti lake kuchelewa kukamilika kwa mwaka wa tano sasa wakati tuhuma zake ni uchochezi wa kigaidi katika mtandao wa Facebook.

Malalamiko hayo yalitolewa jana wakati mtuhumiwa akiwa gerezani, huku Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mmbando na Wakili wa Serikali, Esther Martine wakiwa katika ukumbi uliopo Mahakama ya Kisutu.

Wakili wa Serikali, Esther alidai mara ya mwisho alimfahamisha mshtakiwa Mkuki kwamba upelelezi umekamilika na barua imeandikwa kwenda upelelezi kwa ajili ya maelekezo, tarehe ijayo watakuwa na majibu.

Akijibu, mshtakiwa huyo alidai taarifa hizo si za kweli kwani tangu Agosti mwaka jana amekuwa akiambiwa jalada liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.

“Kiukweli kesi ina muda mrefu, mwaka wa tano, kesi yenyewe ya uchochezi wa kigaidi uliofanyika Facebook.

“Wanatoa taarifa si za kweli, shtaka lenyewe kosa linadaiwa kutendeka Facebook, inashangaza mpaka leo washindwe kuthibitisha kosa lilitendekaje,” alidai mshtakiwa.

Wakili Esther alijibu kwa kudai wakati anatoa taarifa jalada lilikuwa linaenda upelelezi na lipo huko kwani alilifuatilia.

 Aliomba apewe muda wa kufuatilia lilipo ili lisikae sana sababu kesi ni ya muda mrefu na aliomba kesi iahirishwe.

Hakimu Mmbando aliamuru Jamhuri kufuatilia jalada hilo na tarehe ijayo watoe taarifa limefikia hatua gani. Kesi iliahirishwa hadi Januari 23.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles