23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

SHULE YA WANAFUNZI WALIOFANYA VURUGU YAFUNGWA SIKU 14

Na Omary Mlekwa, Hai 

Serikali imeifunga Shule ya Sekondari ya Lyamungo kwa zaidi ya wiki mbili baada ya wanafunzi wake kufanya vurugu na uharibifu katika nyumba ya mwalimu wa nidhamu wakipinga mwenzao kufukuzwa.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Onesmo Buswelu amesema lengo la kuifunga shule hiyo ni kuepusha uharibu zaidi na uvunjifu wa amani.

Amesema vurugu hizo zinatokana na mwanafunzi wa Kidato cha Tano, Moses Siima anayesoma mchepuo wa HGE, anadaiwa kuwatukana walimu jambo ambalo lilisababisha kuadhibiwa pamoja na kusimamishwa masomo.

“Hawa wanafunzi walifanya vurugu na maandamo Februari 28, mwaka huu kwa lengo la kumwona mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya kutokana na mwanafunzi mwenzao kuadhibiwa na mwalimu wa Nidhamu wa shule hiyo, Safari Rasini.

“Kamati ya Ulinzi na Usalama, imeridhia wanafunzi wote kuondoka shuleni na wanapaswa kurejea shuleni Machi 18, mwaka huu,” amesema.

Soma zaidi…

WANAFUNZI WABOMOA NYUMBA YA MWALIMU, WADAI KUCHOSHWA NA VISA VYAKE

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles