26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima vya maji

MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Time to Help limekabidhi visima vitatu kwa shule tofauti za Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mpango wa taasisi hiyo kusaidia shule za msingi na sekondari nchini katika kukabili changamoto tofauti.

Akizungumza jana mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa shule za sekondari Kibwegere, Kibweheri na shule za msingi Kibwegere, mkuu wa tasisi hiyo, Kubilaty Talu alisema wametoa msaada huo baada ya kuombwa kufanya hivyo.

Alisema tasisi hiyo imelenga kuzisaidia shule mbalimbali nchini kukabili changamoto ya mahitaji ya maji na visima hivyo anaamini vitabadili mazingira na kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule hizo tatu ambazo pia zilipewa zawadi za madaftari.

Awali Naibu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya, alisema visima hivyo vitasaidia mengi ikiwa ni pamoja na kulinda afya za watoto kutokana na uhaba wa maji, hivyo pia kuwaepusha na magonjwa yanayotokana na uhaba wa maji safi na salama.

Katika risala ya wanafunzi wa shule hizo ambayo iliwasilishwa kwa mtindo wa ngonjera, waliomba msaada wa vyumba zaidi vya madarasa kutokana na uhaba uliopo na wameshukuru kupata huduma ya maji.

Walisema ukosefu wa maji safi na salama ulisababisha baadhi ya wanafunzi kuugua magonjwa ya matumbo mara kwa mara kutokana na kutumia maji ya kunywa yasiyo safi wala salama.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,400FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles