28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Shirika lajitolea kupima satarani bure

Na  AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM

KUTOKANA na kuongezeka kwa ugonjwa wa saratani ya matiti,shirika lisilo la kiserikali la Associazione Ruvuma Onlus Tanzania, limesema linaanza kampeni ya kupambana na saratani kwa kuhamasisha watu kupima afya zao bure.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam  jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Happy Rwechungura alisema upimaji huo,utahusisha saratani ya tezi dume ambayo imekuwa ikiwasumbua zaidi wanaume.


“Kuna haja ya Watanzania kukumbatia utaratibu wa kupima afya zao na kuzuia magonjwa mapema, badala ya kusubiri kushambuliwa na maradhi na kutafuta tiba kwa kutambua hilo sasa tumejitolea kutoa matibabu ya bure.

“Kuwaona wataalamu mapema kunaweza kusaidia katika hatua za awali za magonjwa kuweza kudhibiti na kuyatibu mfano ugonjwa wa saratani hasa hii ya matiti ukiwahi katika hatua za awali  unaweza kutibiwa  na ukapona ,”alisema.


Alisema wataanza kampeni ya uchunguzi katikati ya mwezi huu hadi Februari, mwakani  kwa lengo la kuokoa maisha ya wananchi wengi ambao wanapambana na saratani  bila ya wao kujijua.


alisema shirika litaweka kambi kituo cha Jamii cha GDB,Tegeta Kwa Ndevu kuanzia kesho na watafanya shughulihiyo kwakutwa nzima.


“Ili  kufanikisha kufanya uchunguzi na kutoa tiba, taasisi yetu itashirikiana na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam kupitia kitengo cha afya…vituo vingine ambavyo vitashiriki ni Tegeta Mission Dispensary, Hospitali ya Edward Muchaud, Hospital ya Sinza, Consolata Mbagala Dispensary, Mbagala Mission na Hospitali ya
Cardinal Rugambwa, Ukonga,”alieleza Rwechungura.


Alisema taasisi hiyo, imekuja na mpango wa kusaidia Serikali katika afya, baada ya kubaini wananchi wanataka huduma ya uchunguzi, lakini hawaipati kwa sababu ya ughali wake.
Alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika uchunguzi wa saratani ya matiti na  tezi dume.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,908FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles