26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Mhadhiri ustawi wa jamiiashikiliwa tuhuma za rusha

Na MWANDISHI WETU-ARUSHA

MHADHIRI Msaidizi wa Chuo cha  Maendeleo ya Jamii Tengeru, Haliye Mabakwe (32),amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashtaka mawili, likiwemo la kuomba rushwa ya Sh 450,000 kwa wanafunzi ili awafaulishe katika mitihani ya marudio.

Jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Martha Mahumbuga,Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU),Richard Jacopiyo, alidai kosa la kwanza, ni mshtakiwa  kujihusisha na vitendo vya rushwa kati ya Septemba 9 na 15, mwaka huu, akiwa eneo la Tengeru chuoni hapo.

“Mshtakiwa akiwa mwajiriwa wa chuo, aliomba rushwa ya shilingi 450,000 kutoka kwa mwanafunzi Joyce Deogratias ambaye alikuwa akikusanya na za wanafunzi wenzake wane wanaosoma chuoni hapo ili awasaidie kufaulu mitihani yao (Supplementary Exams),”alidai

Alidai shtakala la pili  ni kujihusisha na vitendo vya rushwa, ambapo kati ya Septemba  9 hadi 15, mwaka huu   alipokea rushwa ya Sh 449,000 kutoka kwa  Joyce za wanafunzi wanne kwa lengo la kuwafaulisha kwenye masomo yao waliyofeli.

Mshtakiwa  alikana mashtaka hayo, huku Wakili Jacopiyo akiomba mahakama kuahirisha shauri hilo kutokana na upelelezi wake kutokamilika.

Mshtakiwa  aliachiwa kwa dhamana na Hakimu Mahumbuga kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 8, 2020, itakapotajwa tena.

Awali taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkuu wa Takukuru mkoani hapa,Frida Wikesi ilidai  mshtakiwa  alikuwa akiwashawishi wanafunzi wake wa astashahada mwaka wa mwisho kumpatia rushwa ya fedha ili awafaulishe katika somo la Participatory Research Methods,ambalo yeye hufundisha.

“Uchunguzi wa Takukuru, umebaini mtuhumiwa  alikuwa akiwaomba shilingi 50,000 kila mwanafunzi ambaye hakufaulu katika mitihani ya somo hilo,ushawishi aliokuwa akiufanya kupitia mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akipokea fedha hizo kwa wanafunzi wenzake na kuzituma kwa mwalimu huyo kwa miamala ya simu na benki,”ilidai taarifa hiyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles