25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tatizo la udumavu lapungua Tanga

Na Amina Omari,Tanga

TATIZO la udumavu mkoani Tanga, limepungua kutoka asilimia 39 mwaka janahadi kufikia asilimia 34.9 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kikao kazi cha maofisa lishe ngazi ya jamii jana,Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa alisema mikakati ya kupunguza udumavu umesaidia kuanza kupata matokeo ya haraka.

Alisema uwapo wa maofisa lishe hadi ngazi ya jamii, umesaidia kubaini watoto wenye utapiamlo mapema na kuwaanzishia tiba.

“Lishe ni jambo muhimu  katika ukuwaji wa mwili na akili,ukosefu unaweza kuleta athari kwa mtoto na jamii,”alisema.

Aliwataka maofisa kuhakikisha wanafanyakazi ya kuwatambua watoto wenye utapiamlo mlo ngazi yajamii .

Ofisa Lishe Jiji la Tanga, Sakina Magadi alisema  uwapo wa bajeti umesaidia kwa kiasi kikubwa kutekeleza afua za lishe.

“Mwaka jana pekee, tulingewa bajeti ya shilingi milioni 46 ambazo zimefanya shughuli mbalimbali, ikiwamo kuwajengea uwezo maofisa wetu ngazi ya jamii”alisema Magadi.

Alisema wasimamizi wameweza kuwa msaada mkubwa kuwatambua kwa wakati watoto wenye utapiamlo mlo na kuwasaidia tiba mapema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles