Shikalo: Sijagoma kuongeza mkataba Yanga

0
453

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kipa wa Yanga, Farouk Shikalo, ameweka bayana kuwa hajagoma kuongeza mkataba mpya na kwa sasa anaelekeza nguvu katika mechi ya Ligi Kuu zilizobaki na mechi ya nusu fainali ya kombe la shirikisho la Azam.

Shikalo ambaye mkataba wake unafikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu, amesema taarifa zinazosambaa si za kweli.

“Hizi ni rumors tu zinasambazwa na watu tu mitandaoni, kwa sasa nguvu naelekeza kwenye michezo ambayo imebaki ya ligi kuu na FA,” amesema Shikalo akijibu maswali anayoulizwa na mashabiki wa kikosi hicho kupitia mitandao yake ya kijamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here