‘Sheria ya manunuzi iangaliwe upya’

0
563

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Bunge limeombwa kupitia upya kwa kuifanyia mabadiliko Sheria ya manunuzi ya mwaka 2011 kwa sababu ina urasimu mwingi na inajenga mazingira ya rushwa.

Hoja hiyo ilitolewa Dar es Salaam leo Oktoba 29 na mwanasheria wa Kituo cha Taarifa kwa wananchi Tanzania (TCIB), Neema Kimambo ambapo amesema, kuna umuhimu wa sheria hiyo kurekebishwa ili iendane na karne ya 21.


Neema alisema sheria hiyo imejaa mlolongo mrefu wa bodi zinazohusika kwenye suala la tenda na manunuzi na kusababisha kuwapo mazingira ya rushwa na ucheleweshaji wa zabuni hivyo kukwamisha na hatimaye kuchelewesha maendeleo ya wananchi.

“Ni vema sasa tukawa na mlolongo mfupi wa manunuzi kwa kupunguza taasisi zinazohusika katika mchakato mzima wa utoaji zabuni nchini, wote tunajua pesa nyingi za watanzania zinakwenda kwenye miradi ya ujenzi lakini huko pia hakuna uwazi, ufuatilia michakato ya tenda utaona kumejaa vikwazo ambavyo vingi ni visabishi vya rushwa” alisema Neema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TCIB, Deus Kibamba amesema wameandaa ripoti maalum ambayo wataipeleka kwa wabunge kuwakumbusha wajibu wao wa kuisimamia serikali.

Kibamba ambaye ni mwanaharakati amesa “tunatarajia kukutama na wabunge kuwakumbusha wajibu wao lakini zaidi watusaidie kudhibiti matumizi ya serikali kupitoa sheria ya manunuzi.

” Tunalenga hoja nzito na tutawaambia haturidhishwi na mapambano dhidi rushwa kwa sababu utaratibu wa manunuzi haufuatwi” amesema Kibamba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here