Mwanamuziki wa nchini Uingereza, Ed sheeran ametajwa kuwa ndiye msanii tajiri zaidi katika kundi la watu maarufu wenye umri wa chini ya miaka 30.
Utajiri wa Ed sheeran umeongezeka karibu mara
mbili ndani ya miezi 12 ambapo inakadiriwa kuwa paundi milioni 170 na hivyo
kumfanya afanikiwe kumnyang’anya nafasi ya kwanza mwanamuziki Adele.
Nafasi ya pili imechukuliwa na muigizaji wa filamu Daniel
Radcliffe ‘Harry Potter’ ambaye thamani yake ni paundi milioni 90.
Nafasi ya
tatu imechukuliwa na mwanamuziki Harry Styles ambaye alikuwa katika kundi
maarufu la muziki nchini humo la One Direction ambaye anakadiriwa kuwa na
thamani ya paundi milioni 64.
Mwaka jana Adele alishika nafasi ya kwanza akiwa na thamani
ya paundi milioni 147.5 lakini yeye alitimiza miaka 31 Mei 5 mwaka huu na hivyo
hakupata nafasi ya kushirikishwa katika awamu hii.