24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

THE RIGHT WAY, ACTION FOR CHANGE KUELIMISHA JAMII KUELEKEA CHAGUZI ZIJAZO

BRIGHITER MASAKI – DAR ES SALAAM

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Action for Change (ACHA) na The Right Way (TRW) yamepanga kutoa elimu ya uraia na uangalizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi ujao, mpango ambao pia umeulenga Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

Lengo la mpango huo utakaozinduliwa Ijumaa ya wiki hii ni kuzifanya chaguzi hizo kuwa huru, haki na zenye kuaminika kwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mwenyekiti wa TRW, Sebastian Masaki, anasema asasi hizo zimeungana baada ya kupata kibali cha kuendesha shughuli hizo kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

“Asasi hizi zina mwelekeo wa kufanya shughuli zinazofanana, hususan za uchaguzi kikatiba kwa kuhakikisha uendeshaji bora na michakato ya uchaguzi na uungaji mkono wa mabadiliko ya kiutawala kupitia elimu ya uraia.

“Muungano huu utakuwa chombo ambacho kitapunguza gharama na kuchangia thamani ya pesa na kuongeza mbinu za kiufundi na mtaji wa watu kuelekea shughuli hii. Tunatamani kuona mchakato wa uchaguzi ambao unaongozwa na wananchi, kwa maana ya ushirikishaji, yenye uwazi, huru na haki na unaoaminika juu ya misingi ya haki na uwajibikiji.

“Wananchi watashiriki mchakato na zoezi ambalo hali za binadamu na misingi yake vitatamalaki. Katika jamii inayofuata mishingi ya demokrasia ya uchaguzi ni kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi wa  Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020 ni huru, haki na wenye kuhaminika,” alisema Masaki.

Aliongeza ACHA na TRW watatoa elimu ya uraia kwa mpiga kura na uangalizi wa michakato ya chaguzi kwa kuzingatia vigezo na kanuni za Tanzania na zile za kimataifa.

“Elimu hiyo itatolewa kupitia vyombo vya habari na mawasiliano ya aina nyingine. Uangalizi au uchambuzi wa mifumo ya uchaguzi vitakwenda sanjari ili kuziwezesha ACHA na TRW kubaini ukiukwaji wa kanuni za mchakato wa uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles