Sheikh: Waislamu tufanye kazi

Mohamed Mwansasu
 Mohamed Mwansasu
Mohamed Mwansasu

Na Pendo Fundisha, Mbeya

SHEIKH wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mwansasu, amesema Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, haiendekezi siasa hivyo kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kuachana  na tabia ya ushabiki wa vyama vya siasa ili wafanye kazi za maendeleo.

Alisema wakati wa porojo za kisiasa umepita, kilichobaki kwao ni kufanya kazi kwa kujituma zaidi ili kuondokana na utegemezi ambao umekuwa ukipigwa vita.

Changamoto hiyo imetolewa na Sheikh Mwansasu, wakati wa hotuba ya sikukuu ya Idd El-Fitri iliyosomwa katika Msikiti Mkuu wa Al-Masjid L-I Jumatano.

Sheikh Mwansasu alisema Serikali ya Magufuli, imeanza  kwa hatua ya utendaji kazi mzuri ambao umeonekana kukidhi huduma zinazolenga mahitaji ya wananchi.

Alisema wananchi walikuwa wakihitaji kiongozi  mwajibikaji, mchapakazi na mwadilifu jambo ambalo limeonekana kwa Rais Magufuli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here