Wajasiriamali wakopeshwa mil 52/-

0
556
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Raphael Kimary
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Raphael Kimary
Raphael Kimary

NA AMON MTEGA, SONGEA

HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, imetoa mkopo wa Sh milioni 52 kwa vikundi 107 vya wajasiriamali ili kuendeleza miradi yao.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya vikundi hivyo juzi, Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Raphael Kimary, aliwaasa wajasiriamali hao kuwa na nidhamu ya matumizi ya mikopo ili mwisho wa siku wahakikishe wanairejesha kwa wakati.

Alisema mkopo huo umetolewa na manispaa kwa lengo la kusaidia vikundi vya wajasiriamali  katika shughuli za uwekezaji  na kuhakikisha wanainua kipato chao cha kila siku.

Kwa upande wake Ofisa Maendeleo ya Jamii wa manispaa hiyo, Naftali Saiyoloi, alisema mkopo huo una lengo la kuinua hali ya uchumi katika makundi hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here