31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

SHAHIDI: WEMA ALINIAMBIA ANAVUTA BANGI KAMA STAREHE

Na Kulwa Mzee , Dar es Salaam

Mpelelezi katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Msanii wa filamu, Wema Sepetu, WP Marry amedai mahakamani kwamba msanii huyo alimwambia hajihusishi na kuuza dawa za kulevya ila anatumia bangi kwa starehe.

Mary ambaye shahidi katika kesi hiyo, amedai hivyo leo Jumatatu Februari 26, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akitoa ushahidi akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Amedai Wema Februari 4, mwaka jana wakiwa ndani ya gari la polisi wakitokea Kituo Kikuu cha Polisi kuelekea nyumbani kwake Bunju Basihaya kwa ajili ya upekuzi ndipo alipomweleza hayo baada ya kumuuliza kama anahusika na kutumia dawa za kulevya ama kuuza.

“Wema alidai hajihusishi na kuuza ila anatumia bangi kama starehe pia alidai mara ya mwisho kuvuta ilikuwa jumatatu na siku hiyo ilikuwa Jumamosi,” amedai shahidi huyo.

Amedai kwa kuwa alikuwa anaongea na Wema hadhani kama askari wengine waliokuwapo kwenye gari walisikia, ila baada ya kuona Wema amekiri alimweleza OC CID Dennis Mujumba wakiwa ndani ya gari.

Wema anatuhumiwa kwa kosa la matumizi ya dawa za kulevya ikiwamo bango. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Machi 12 na 13, mwaka huu kwa ushahidi wa upande wa jamhuri kuendelea na mashahidi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles