22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

IGP SIRRO AONYA WANAOTAKA KUANDAMANA

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewaonya wanasiasa ambao wamepanga kuandamana nchi nzima kwani jeshi lake limejipanga kukabiliana nao.

Akizungumza jana mkoani Simiyu leo Jumatatu Februari 26, IGP Sirro amesema kuwa jeshi hilo limepata taarifa kutoka katika vyanzo vyake juu ya kuwepo kwa makundi ya vijana ambao wanajiita Wanamapinduzi waliopanga kuandamana nchi nzima chini ya uratibu wa chama kimoja cha siasa ambacho hakukitaja.

“Yeyote atakayeandamana au atakayebainika akiwa katika mikakati ya maandamano atashughulikiwa sisi wamejipanga kikamilifu kukabiliana na wandamanaji ikiwa ni pamoja na kuwakamata watu wote watakaoandamana.

“Tumeshapata taarifa kuwa kuna vijana wanajipanga kuandamana nchi nzima sisi kama jeshi la polisi tumejipanga vyema kuhakikisha tunawadhibiti wasiweze kufanya chochote  na mtu yoyote ambaye ataandamana tutamchukulia hatua za kali za kisheria,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles